Ministry of Foreign Affairs Under Fire
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni kwa mara nyingine imejipata mashakani kuhusiana na uuzaji wa mali ya kenya mjini Lagos, Nigeria.Hii ni baada ya kubainika kwamba shilingi milioni 8.4 zilizotokana na mauzo hayo hazijulikani ziliko. Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu ulinzi na mashauri ya nchi za kigeni, gavana wa benki kuu prof. Njuguna Ndung’u, alidhibitisha kuwa kiasi cha pesa walichopokea kutoka kwa balozi wa kenya nchini nigeria ni chini ya kiwango walichotarajia kutokana na mauzo hayo. Akiwa ameandamana na mkurugenzi wa huduma za benki gerald nyaoma, Ndung’u hata hivyo alisema kuwa sio jukumu la benki hiyo kufanya uchunguzi kuhusu kutoweka kwa pesa hizo. Kamati hiyo tayari imekutana na maafisa kutoka wizara ya mashauri ya nchi za kigeni, lakini dosari hiyo haikuelezewa au kubainika ikiwa balozi wa Kenya nchini Nigeria alihojiwa kuhusiana na kisa hicho.
-------
The Ministry of foreign affairs is once again on the spot over the handling of the sale of a government property in Lagos after new revelations that 8.4 million shillings from the sale cannot be accounted for. Appearing before the Parliamentary Committee on Defense and Foreign Relations, Central Bank governor Njuguna Ndung’u confirmed that the money they received from the Ambassandor in Nigeria was less the sale figure the Ministry had stated. Backed by the Director of Banking services the Gerald Nyaoma the governor however said it was not CBK’s responsibility to query the discrepancy.